Tunafanya
Uhifadhi
Ufanikiwe katika
Ardhi ya Jamii

MAHALI AMBAPO WATU WA ENEO HUSIKA WANAONGOZA,
UHIFADHI HUSTAWI.
TUNAWASAIDIA KUFANIKISHA HILO.

Honeyguide, tumejizatiti katika dira yenye nguvu kwa ajili ya Tanzania: kuwezesha jamii kumiliki, kuongoza, na kusimamia rasilimali zao asilia.

Dhamira yetu kuu ni kuufafanua upya uhifadhi kama nguvu inayojitegemea inayochochea ustawi wa pamoja, na kuhakikisha kuwa watu na wanyamapori wanaendelea kustawi kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Tunafanikisha hili kwa kuimarisha utawala, usimamizi na biashara za maeneo haya ya uhifadhi yanayoongozwa na jamii, ili yaweze kustawi kama biashara za kijamii zinazojitegemea na zinazotoa manufaa ya kiuchumi, kijamii na kiikolojia kwa jamii za maeneo husika.

TUNAELEKEZA SHUGHULI NA UWEKEZAJI WETU KATIKA MAENEO YA UHIFADHI YANAYOMILIKIWA NA KUSIMAMIWA NA JAMII TU, IKIWEMO JUMUIYA ZA HIFADHI ZA WANYAMAPORI (WMAs).

Changamoto

60%

YA WANYAMAPORI WANAPATIKANA KATIKA ARDHI ZA JAMII

Mifumo ya kiikolojia hustawi pale jamii zinapoona thamani halisi na ya kudumu ya kuishi pamoja na wanyamapori.

Hata hivyo, Maeneo haya ya Uhifadhi yanayoongozwa na Jamii mara nyingi hukosa ujuzi wa kibiashara na msaada unaohitajika ili kujiendesha kwa mafanikio kama biashara za kijamii. Changamoto kubwa ni ugumu wa mifumo ya utawala na usimamizi, pamoja na ukosefu wa miongozo iliyo wazi na rahisi kueleweka kwa ajili ya kuendesha maeneo haya kwa ufanisi.

TUNACHOFANYA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ILIYOPO

TUNAWAJENGEA uwezo viongozi wa jamii husika

za Maeneo ya Uhifadhi wa Jamii, kwa kuwapatia wajumbe wa vyombo vya uongozi maarifa na stadi zinazowawezesha kuelewa majukumu yao, kufanya maamuzi sahihi, na kutekeleza misingi ya utawala bora inayozingatia uwazi, uwajibikaji na usawa, ili kujenga na kuendesha kwa mafanikio biashara za kijamii zinazoongozwa na jamii.

Tunakuza usimamizi wa KITAALAMU

wa maeneo ya uhifadhi ya jamii kwa kuimarisha uwezo wa timu za WMAs kuendesha shughuli za kila siku kwa ufanisi na tija. Kupitia matumizi ya mifumo na nyenzo katika maeneo nane muhimu ya usimamizi ikiwemo fedha na utawala. Tunasaidia kujenga biashara za kijamii zilizo imara, endelevu, na zinazoongozwa na jamii.

JINSI TUNAVYOFANYA

KUJUMUISHA UTAALAMU NA

UWEKEZAJI

Honeyguide Foundation tunaleta pamoja maarifa ya kitaalamu, yakiwemo maarifa kutoka kwa wanajamii wa maeneo husika, pamoja na uwekezaji mkubwa, zana bunifu, na ushirikiano wa kimkakati ili kujenga Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori zilizo imara, zenye ufanisi, na endelevu.

JINSI TUNAVYOPIMA MAFANIKIO

TULITENGENEZA ZANA YA KUJITATHMINI INAYOZISAIDIA JAMII KUFUATILIA MAENDELEO YAO KATIKA NYANJA NNE MUHIMU.

Zana hii inahakikisha kuwa WMAs zina msingi imara wa kiikolojia, ambapo wanyamapori na makazi yao yanalindwa ipasavyo. Pia inahakikisha kuwa WMAs zinathaminiwa na jamii kwa kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika kikamilifu, wana imani na WMAs, na wanaona thamani ya uwepo wa WMAs. Tunasaidia WMAs kujenga uwezo wa kifedha ili ziweze kuzalisha mapato ya kutosha kugharamia shughuli zake za kila siku na kuchangia miradi ya maendeleo ya jamii. Aidha, zana hii hupima ustahimilivu wa biashara kwa kutathmini uwepo wa utawala bora na usimamizi wa kitaalamu unaohitajika kwa mafanikio ya biashara za kijamii zinazoongozwa na jamii.

MAFANIKIO YETU

13

â—Ź â—Ź â—Ź

Tunazijengea uwezo Jumuiya 13 za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs) zinazomilikiwa na jamii nchini nchini Tanzania

1,900,000

â—Ź â—Ź â—Ź

Kulinda hekta milioni 1.9 za ardhi kwa ajili ya wanyamapori na makazi asilia.

+500,000

â—Ź â—Ź â—Ź

Kazi yetu inanufaisha zaidi ya watu laki tano kwa kuunganisha uhifadhi wa mazingira na maendeleo endelevu yenye manufaa ya kudumu kwa jamii.

MAENEO TUNAYOFANYA KAZI

Tunafanya kazi katika maeneo ya uhifadhi yanayoongozwa na jamii nchini Tanzania

Honeyguide inafanya kazi kwa kiwango chenye umuhimu wa kitaifa, kwa kushirikiana na jamii za maeneo husika kulinda eneo la ardhi linalokadiriwa kuwa sawa na takriban asilimia 2.4 ya eneo lote la Tanzania. Kwa kiwango hiki, matokeo ya kazi yetu yanazidi manufaa ya maeneo husika pekee; yanachangia kuimarisha muunganiko wa mifumo ya kiikolojia katika maeneo mbalimbali, kuongeza uwezo wa kuhifadhi kaboni, na kusaidia kufikiwa kwa malengo ya kitaifa ya uhifadhi wa mazingira na wanyamapori.

Watu Tunaofanya Nao Kazi

Mkakati wetu wa miaka 5

Mpango Mkakati Wetu wa Miaka 5 (2022-2026)

Mpango Mkakati wetu wa Miaka Mitano unafafanua dira, madhumuni na mwelekeo wa kazi yetu katika miaka ijayo. Mpango huu unaainisha malengo yetu mawili makuu, sababu zilizotufanya kuyachagua, matokeo na athari chanja tunazolenga kufikia, pamoja na wadau na washirika watakaoshirikiana nasi katika safari hii ya kuleta mabadiliko chanya.

Habari Zetu Mpya