Mwindaji haramu ahukumiwa jela kwa kumiliki mzoga wa tembo na pembe za ndovu

Mtu aliyekuwa anakabiliwa na mashtaka ya kumiliki mzoga wa tembo na kumiliki pembe za ndovu amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kila moja ya makosa hayo mawili. Lobulu Mapengo, aliyekamatwa mwaka jana katika kata ya Mto-wa-Mbu, Wilaya ya Monduli, alihudhuria mahakamani kwa mara ya kwanza mnamo Agosti 2015. Alikamatwa na kushtakiwa Julai iliyopita pamoja