Afisa wa Utalii wa Honeyguide, Komolo Simel, anaandaa mashindano ya baiskeli yatakayofanyika katika WMA ya Enduimet. “Lengo letu ni kutoa uelewa kuhusu shughuli za utalii za ajabu zilizopo Enduimet na kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia WMA katika kuhifadhi wanyamapori na maliasili zake….” alisema afisa huyo.

Waandaaji wa Honeyguide kwa ajili ya tukio hili tayari wamekutana na klabu ya uendeshaji baiskeli ya Arusha ili kupata washiriki na njia zitakazotumika. Kwa sasa, klabu ya uendeshaji baiskeli ya Moshi imeombwa kuhudhuria mashindano hayo.

Hata hivyo, mipango mingi kwa ajili ya tukio hili bado haijaamuliwa, ikijumuisha; ramani ya mtandaoni kwa ajili ya njia na uthibitisho kutoka kwa klabu ya uendeshaji baiskeli ya Moshi, lakini tukio hili linatarajiwa kuzinduliwa kati ya Julai au Agosti 2016. Mnakaribishwa wote kushuhudia ziara ya kwanza kabisa ya uendeshaji baiskeli upande wa Magharibi mwa Kilimanjaro huku mkifurahia wingi wa wanyamapori kwenye miteremko mikali!