Kuufanya Uhifadhi
kuwa Biashara
Stahimilivu
inayomilikiwa na Jamii
Shughuli tunazofanya

Kama wachochezi wa maendeleo, tunasaidia WMAs zinazomilikiwa na jamii kukua na kuimarika kuwa taasisi za kijamii imara na zinazojitegemea.
Mfumo endelevu unaojigharamia wenyewe, unaoleta manufaa kwa jamii na kulinda makazi ya asili pamoja na wanyamapori kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Kwa zaidi ya muongo mmoja, tumejenga mfumo unaolinda mazingira ya asili nje ya hifadhi za taifa kwa kuimarisha kila nyanja ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori. Kuanzia utawala bora na usimamizi, ulinzi wa maliasili, kupunguza migogoro kati ya binadamu na wanyamapori (HWC), hadi maendeleo ya biashara za kijamii. Athari chanya zetu za muda mrefu zinachochewa na ubunifu endelevu, ushirikiano imara, uchechemuzi wenye mwelekeo mahsusi, na mifumo madhubuti inayohakikisha kazi yetu inakuwa yenye ufanisi, inayoweza kupanuliwa kwa kiwango kikubwa, na yenye uwezo wa kudumu kwa muda mrefu.
Uhifadhi unaoongozwa na Jamii
Honeyguide inaamini kuwa mustakabali wa maeneo ya asili barani Afrika unategemea suluhisho linaloongozwa na jamii, ambapo jamii za wenyeji ndizo zinazoongoza juhudi za uhifadhi. Jamii zinapopewa nyenzo sahihi, rasilimali na msaada unaohitajika, huwa na uwezo, ujuzi, uhusiano na maarifa ya asili ya kusimamia maeneo ya uhifadhi na kulinda rasilimali zao za asili. Ili mfumo wa uhifadhi unaoongozwa na jamii uweze kufanikiwa, ni muhimu mipango na shughuli za uhifadhi zimilikiwe na kuongozwa na jamii husika ili ziwe endelevu kwa muda mrefu.
Programu Zetu
Programu zetu huimarisha kila nyanja ya uhifadhi unaoongozwa na jamii, kuanzia utawala bora na usimamizi, maendeleo ya biashara, ulinzi wa maliasili, hadi upunguzaji wa migogoro kati ya binadamu na wanyamapori (HWC). Juhudi hizi zilizounganishwa husaidia Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs) kuwa imara zaidi, zenye ustahimilivu mkubwa, na kujitegemea kwa kiwango kikubwa zaidi.
Vichocheo vya Kimkakati
Ubunifu, ushirikiano, uchechemuzi, na mifumo imara ndiyo vinavyowezesha kazi za Honeyguide kutekelezwa kwa mafanikio. Vichocheo hivi vya kimkakati vinahakikisha kuwa uhifadhi unaoongozwa na jamii unakuwa wenye ufanisi, unaoweza kupanuliwa kwa kiwango kikubwa zaidi, na wenye uwezo wa kudumu kwa muda mrefu.
Habari Zetu Mpya
Jamii za ndani ni rasilimali ya uhifadhi isiyothaminiwa vya kutosha (maoni)
Suala si kujitolea au mtaji, bali ni kutoelewana jinsi uhifadhi unavyofanya kazi. Mbinu zinazoongozwa na jamii ni za ufanisi zaidi na zenye ustahimilivu kwa sababu zinaweka mamlaka kwa wale walio karibu zaidi na ardhi.
Kujenga Nguvu ya Pamoja kwa Utawala wa Haki
"Sheria inasema tunapaswa kuwepo," kikundi kimoja cha wanawake kilifikiria wakati wa kikao cha makundi madogo, "lakini chumba cha kufanya maamuzi bado kinapata njia za kutufukuza."
Ubunifu Unaotoa Matokeo: Mawazo Madogo, Athari Kubwa
Wanasema haja ni mama wa ubunifu, na kwa WMA zinazokabiliwa na changamoto zinazozidi na rasilimali chache, kuwa na ubunifu haikuwa chaguo; ilikuwa ni lazima.




