Utawala
unaobadilisha
tabia
si miundo tu.
Utawala
Mafunzo yetu ya utawala bora na uwezeshaji vinalenga kuleta mabadiliko ya tabia, si kuanzisha mifumo pekee.
Utawala bora ni muhimu katika kuhakikisha uwazi na usawa katika Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs).
Kwa kuimarisha uongozi, uwezo wa kufanya maamuzi na uwajibikaji, jamii zinaweza kusimamia kwa uwazi rasilimali na mapato yao, na kuhakikisha kuwa manufaa yanagawanywa kwa usawa miongoni mwa wanajamii wote. Mifumo iliyo wazi hupunguza migogoro, hujenga imani, na huonyesha kwa wadau wa ndani na washirika wa nje kuwa WMA inasimamiwa kwa ufanisi na weledi. Hili sio tu linaziwezesha jamii, bali pia huweka msingi imara wa maendeleo endelevu na mafanikio ya muda mrefu katika uhifadhi.
Kazi yetu ya kukuza utawala bora inawawezesha viongozi wa biashara hizi za kijamii
Kwa kuwapatia ujuzi, maarifa na imani ili kufanya maono yao ya usimamizi wa maliasili kuwa hatua za vitendo zinazoboresha maisha ya jamii. Kwa kuimarisha uongozi, usimamizi wa fedha na uwezo wa kufanya maamuzi, tunahakikisha kuwa jamii zinaweza kusimamia rasilimali zao kwa njia endelevu, kuzalisha manufaa ya kiuchumi, na kujenga taasisi za uhifadhi unaoongozwa na jamii zinazojitegemea na zenye uwezo wa kudumu kwa muda mrefu.
Uchambuzi wa kina kuhusu Makame WMA; Jinsi utawala bora unavyochangia ustawi wa jamii.
Nini hutokea pale ambapo utawala bora unafanya kazi kwa vitendo? Makame WMA inatuonyesha.
Jumuiya ya Hifadhi ya Wanymapori Makame inaonyesha kwa nini Honeyguide inawekeza katika kuimarisha utawala kama msingi wa uhifadhi unaoongozwa na jamii. Kulinda wanyamapori na kuvutia wawekezaji ni muhimu, lakini hilo pekee halitoshi. Ili uhifadhi uweze kudumu, jamii lazima ziziamini taasisi zinazosimamia ardhi yao. Zinapaswa kuelewa jinsi maamuzi yanavyofanywa, kujua ni nani anayewawakilisha, na kuona kwamba viongozi wao wanawajibika.
Makame WMA inaonyesha kile kinachowezekana pale ambapo utawala haupo kwenye sera na kanuni pekee, bali unatekelezwa na kuishi katika utendaji wa kila siku.
Soma zaidi kuhusu athari chanya ambazo mbinu yetu imeleta katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Makame.>
Kuanzia Tathmini hadi Utekelezaji: Kuimarisha Utawala Bora kwa Mzunguko Endelevu
Kazi yetu ya utawala huanza kwa kufanya tathmini ya awali kwa kutumia zana ya SAGE ili kubaini maeneo yenye ubora na yale yanayohitaji kuboreshwa. Kisha tunatoa mafunzo ya msingi na mafunzo mahsusi ya utawala kupitia Mfumo wa Kujenga Uwezo wa Utawala (GCBF), tukiwajengea viongozi uwezo katika usimamizi, uwajibikaji, usimamizi wa fedha na rasilimali watu. Kupitia ufuatiliaji endelevu wa Utawala kwa Vitendo (GIA), tunafuatilia mabadiliko ya mwenendo na kuhakikisha kuwa maboresho ya utawala yanatafsiriwa kuwa maamuzi bora, usimamizi wenye ufanisi, na WMAs zenye nguvu na endelevu.
Tunafanikisha maono haya kwa kuunganisha zana za vitendo, takwimu, na usaidizi wa karibu kwa viongozi wa WMAs, serikali za vijiji, wanajamii na washirika wa kitaifa.
SAGE Kuongoza WMAs Kufikia Mafanikio
Honeyguide hutumia zana ya SAGE kusaidia jamii kutathmini utawala na usawa katika WMAs zao. Kwa kuwaleta pamoja wadau mbalimbali, SAGE hubaini mapungufu, husaidia uandaaji wa mafunzo lengwa na huimarisha usimamizi wa WMAs.
GCBF Kuimarisha Uongozi wa WMA kwa Athari Chanya za Muda Mrefu
Honeyguide hufanya kazi moja kwa moja na viongozi wa WMAs ili kuimarisha namna maamuzi yanavyofanywa, fedha zinavyosimamiwa, na jinsi jamii zinavyowakilishwa. Kupitia Mfumo wa Kujenga Uwezo wa Utawala (GCBF), tunatoa mafunzo kwa vitendo, ushauri elekezi na ufuatiliaji endelevu unaowezesha kanuni za utawala bora kutekelezwa katika shughuli za kila siku. Hii huwasaidia viongozi kusimamia WMAs zao kwa uwazi, uwajibikaji na kwa kuzingatia maslahi ya jamii wanazozihudumia pamoja na uhifadhi wa wanyamapori.
Muundo wa mfumo huu umejengwa katika sehemu kuu mbili: Moduli za Msingi na Moduli Maalum
Moduli za Msingi zinaweka misingi muhimu ya utawala bora. Maeneo haya ya msingi yanajumuisha kanuni za Utawala Bora na Uongozi, mifumo ya Kisheria na Sera, miongozo madhubuti ya usimamizi wa fedha na uwajibikaji, pamoja na viwango vya usimamizi wa rasilimali watu na maadili.
Moduli Maalum huwezesha utoaji wa mafunzo kulingana na mahitaji mahususi ya taasisi. Maeneo haya ya nyongeza yanahusisha mada maalum kama vile usimamizi na utatuzi wa migogoro, kuimarisha usawa wa kijinsia na ujumuishaji wa makundi yote ya kijamii, kuboresha mawasiliano na ushirikishwaji wa wadau, pamoja na mbinu za vitendo za kufuatilia na kutathmini utendaji wa utawala.
Changamoto nyingi za utawala husababishwa na ukosefu wa taarifa sahihi. Honeyguide husaidia WMAs kubuni mifumo ya mawasiliano na usambazaji wa taarifa inayowafikia wanajamii, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), wawekezaji, taasisi za serikali, pamoja na wajumbe wa vyombo vya utawala.
Lengo ni kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayeshangazwa na maamuzi yanayoathiri ardhi yake, haki zake au maisha yake.
Utawala kwa Vitendo (GIA): Kutathmini na kuimarisha utawala
Honeyguide imeandaa Zana ya Tathmini ya Utawala kwa Vitendo (GIA). GIA inawasaidia viongozi wa WMAs kutekeleza kanuni za utawala bora kwa vitendo. Kwa kuunganisha ukaguzi wa mifumo na nyaraka pamoja na maoni kutoka kwa jamii, GIA hubaini maeneo yanayohitaji kuboreshwa katika uongozi, uwajibikaji na ushirikishwaji. Honeyguide hutumia GIA kufuatilia utendaji, kuongoza maamuzi na kujenga utawala bora katika shughuli za kila siku. Hii husaidia WMAs kuwa na uwazi, zinazosimamiwa kwa weledi na zilizo tayari kuvutia uwekezaji, huku zikitoa manufaa halisi kwa jamii na wanyamapori.
GIA hutathmini utawala katika vipengele vitano muhimu: Uwajibikaji, Uwezo, Ushiriki na Kufikia Mwafaka, Uwazi na Upatikanaji wa Taarifa, pamoja na Uendelevu.
Tathmini hii hukusanya mitazamo kutoka kwa wadau mbalimbali, wakiwemo wanajamii, vyombo vya utawala vya WMAs, timu za usimamizi, maafisa wa shughuli za uhifadhi, na wadau wa nje.
GIA inajumuisha mbinu mbili za tathmini:
Kila WMA hupokea dashibodi na kadi za tathmini zinazoonyesha maeneo yenye mafanikio, mapungufu, vihatarishi na hatua za kipaumbele zinazohitaji kuchukuliwa. GIA ni mfumo endelevu wa kujifunza unaotumiwa na WMAs, washirika na serikali kwa kipindi kirefu ili kufuatilia maendeleo na kuendelea kuboresha utawala.
Vipengele vya GIA

Maswali na Majibu








