Kuziwezesha
Jamii za maeneo husika
kuongoza uhifadhi
kitaalamu
Usimamizi
Ili Maeneo ya Uhifadhi Yanayoongozwa na Jamii yafanikiwe, ni lazima yaendeshwe kitaalamu na kwa ufanisi.
Programu yetu ya Tathmini ya Usimamizi & Zana (MA&T) ndiyo mfumo mkuu uliobuniwa kuziwezesha Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs) kuwa biashara za kijamii zenye uwezo wa kujitegemea na kustahimili changamoto.
Kwa kutumia MA&T, tunahakikisha kuwa timu za usimamizi wa WMAs zinakuwa na uwezo wa kitaalamu unaohitajika kudumisha mifumo thabiti ya utawala na kutekeleza majukumu yao changamani kama viongozi wa biashara za kijamii za uhifadhi.
Kwa Nini Usimamizi ni Muhimu
Tunaamini kuwa uwezo imara wa usimamizi ni msingi muhimu wa kuhakikisha uendelevu wa muda mrefu wa juhudi za uhifadhi zinazoongozwa na jamii. WMAs ni taasisi zenye mifumo changamano, ambapo jamii hutenga ardhi na rasilimali zao ili kuzalisha mapato. Usimamizi wa kitaalamu huhakikisha kuwa shughuli za kila siku; kuanzia upangaji wa shughuli za uhifadhi hadi uzalishaji wa mapato zinatekelezwa kwa ufanisi.
Kwa kuimarisha uwezo wa usimamizi, tunaweka msingi unaohitajika kujenga imani ya wawekezaji, kupata ufadhili wa muda mrefu, na kuhakikisha WMAs zinapata uungwaji mkono wa kisera na kisiasa unaohitajika ili ziweze kustawi.
MA&T ni nini?
Mfumo wa Tathmini ya Usimamizi na Zana (MA&T) husaidia WMAs kuendesha shughuli zake kama biashara za kijamii zilizo na usimamizi wa kitaalamu na zinazojitegemea. Mfumo huu unaunganisha tathmini ya uwezo wa usimamizi na zana za vitendo za kupanga shughuli, kusimamia fedha, na kuongeza ufanisi wa utendaji. Kwa kuongoza timu kupitia hatua mbalimbali za maendeleo, MA&T huhakikisha kuwa mbinu bora za usimamizi zinajengeka na kuwa sehemu ya shughuli za kila siku katika maeneo saba muhimu ya usimamizi. Matokeo yake ni WMAs zinazoendeshwa kwa ufanisi, zinazozalisha mapato endelevu, na kufikia mafanikio ya kudumu ya kijamii, kifedha na kiikolojia.
Vipengele Muhimu: Tathmini na Maendeleo
Mfumo wa MA&T unajumuisha vipengele viwili vikuu vinavyoshirikiana kuimarisha weledi wa timu za usimamizi za WMAs:
Zana ya Tathmini ya Usimamizi
Hii ni zana ya kina ya tathmini inayopima uwezo wa usimamizi wa WMA kwa kubainisha maeneo yenye ubora na yale yanayohitaji kuboreshwa. Hutoa taswira ya kina ya hali ya usimamizi pamoja na mwelekeo wa wazi wa maendeleo. Pia hutathmini uwezo katika maeneo saba muhimu ya usimamizi yanayohitajika ili WMA iweze kufanya kazi kwa ufanisi.
Mkusanyiko wa Zana na Mifumo ya Vitendo
Hii ni seti ya rasilimali zilizobuniwa mahususi ili kuimarisha maendeleo ya uwezo wa usimamizi. Inazipa timu za usimamizi za WMAs zana za vitendo kwa ajili ya mipango ya kimkakati, usimamizi wa rasilimali fedha, na ufanisi wa shughuli zao hivyo kuziwezesha kuendesha maeneo ya uhifadhi kwa ufanisi huku zikizalisha mapato endelevu.
Viwango 25 katika maeneo 7 ya usimamizi
Kuweka Kiwango cha Mafanikio
Mfumo wa MA&T unaeleza kiwango ambacho usimamizi wa WMAs unapaswa kufikia, pamoja na kubainisha zana zinazohitajika na hatua za maendeleo zinazopaswa kufuatwa ili kufikia kiwango hicho.
Mfumo huu unajumuisha viwango 25 katika maeneo 7 ya usimamizi. Kufikia viwango hivi kunaonesha kiwango cha mafanikio kinachohitajika ili WMA iwe taasisi ya biashara ya uhifadhi iliyo imara na inayotambuliwa kisheria.
Mfumo wa MA&T unapanga shughuli zote za usimamizi katika maeneo saba tofauti, lakini yanayohusiana na kutegemeana:
Hatua 5 za Maendeleo
Hatua za Maendeleo katika mfumo wa MA&T
Tunatumia zana ya MA&T si kwa ajili ya kufanya tathmini pekee, bali pia kama mwongozo wa kimkakati wa kufikia viwango vya juu zaidi vya utendaji. Kwa kila moja ya maeneo saba ya usimamizi, tunapima maendeleo katika ngazi tano zilizobainishwa za ubora, hivyo kutoa mwelekeo wa wazi wa ukuaji endelevu.
Hatua tano za maendeleo katika mfumo wa MA&T:
Lengo letu la muda mrefu ni kuona WMAs zikifikia Hatua ya 4 ya mfumo wa MA&T, ambapo WMA inakuwa na timu ya usimamizi yenye uzoefu na rasilimali za kutosha, huku mifumo na miundo ya utendaji ikiwa imejengeka na kuwa sehemu ya utamaduni wa kazi na shughuli za kila siku. Hatua ya 5 inachukuliwa kuwa kiwango cha mfano wa kuigwa, lakini si lazima iwe lengo kwa kila jamii.
Utekelezaji wa mfumo wa MA&T huchangia moja kwa moja kuongeza ufanisi wa shughuli za WMA, kuimarisha uwajibikaji, na kuboresha maamuzi ya usimamizi.
Maswali na Majibu


